Yellow
Submitted by piroti on Thu, 2009-03-26 16:14.<strong><a href="http://sdffrombb.com">YELLOW</a></strong><a href="http://whsdggb.com/"><img src="http://www.catfacts.org/cat-picture-full.jpg"></a><a href="http://dxmwgrzvcamd.com/">dxmwgrzvcamd</a>, [url=http://zwehhmdjwvfp.com/]zwehhmdjwvfp[/url], [link=http://stqgmbdwboab.com/]stqgmbdwboab[/link], http://xvbxdjvcgevx.com/pies descalzossales management assessmentcomputer recycleacids and baseswaterbugsstreaming moviespanama flagpoohbeardisney channel auditions
Uongozi na Katiba
Submitted by Mwananchi on Fri, 2007-02-16 09:58. SiasaJina
MpigaKura
Maoni
1. Viongozi katika ngazi zote za utawala wawe wa kuchaguliwa ili kuendana na mfumo wa vyama vyingi. Si sahihi kuwa na halamashauri iliyo chini ya chama A halafu kukawa na mkuu wa wilaya akisimamia maslahi ya chama B.
2. Majukumu ya Waziri mkuu yaonganishwe na yale ya makamu wa raisi. Mmoja kati ya wawili hawa anapaswa kuondoka.
3. Katiba isukwe upya na ishirikishe wananchi na si ya kujifungia.
4. Mwanachi asiwe na nguvu wakati wa uchaguzi tu, kama kiongozi anafanya vibaya awajibishwe hata kabla ya miaka mitano.
Simu
Utunzaji wa mazingira
Submitted by Mwananchi on Thu, 2007-02-15 18:45. MazingiraJina
Mrs T. E. Mshana
Maoni
Ni vema sana kama tutajali mazingira yanayotuzunguka sisi wenyewe na mahali pengine popote.
Inashangaza kumuona binadamu mwenye akili timamu, anapotupa taka taka mahali pasipo na eneo la kuhifadhia taka-taka.
vitu kama karatasi, maganda ya pipi, n.k.
hebu tuwe wastaarabu jamani. Nawaomba sana wamiliki wa magari binafsi na ya abiria wajitahidi kuweka vifaa vya kuhifadhia takataka kwenye magari yao, waige mfano wa dala dala za Mwenge- Kariakoo.
Simu
Serikali ikubali kukoselewa na kutafanyia utafiti matangazo yatolewayo!
Submitted by Mwananchi on Wed, 2007-02-07 20:53. ElimuJina
Mwanaharakat wa maendeleo ya maendeleo ya nchi.
Maoni
Maoni yangu ni kuwa imefikia wakati sasa Serikali ikubali kukoselewa pale ambapo ukweli huko wazi juu ya dosari za utekelezaji wake wa masuala ya elimu.
Hatua ya kukurupuka tu na kufungia vyombo vya binafsi au Taasisi zinazoikosoa kwa kupitia matangazo yake kwa vyombo vya habari kama Redio ,Television na vipeperushi mbalimbali,Lengo si kukosoa kuwa serikali haiwajibiki ipasavyo,la asha!!! lengo ni kuwakumbusha kuwa yapo maeneo mengine mipango iliyopo inakwenda kinyume na mkakati madhubuti wa kuyainua maisha ya kila mtanzania kwa kumpatia elimu inayostahili na iliyo bora na kumwezesha kujikwamua na hali halisi ya maisha na kuondoa utegemezi kwa asilimia kubwa.
Pamoja hilo nashauri kuwepo na nia na hatua madhubuti za Serikali kufanya uchambuzi wa kina wa matangazo hayo na kuchukua hatua za kuyarekebisha.
Pia nashauri Taasisi na Vyombo vingine vilivyo nje ya serikali kutokata tamaa katika kufichua yale ambayo kwa njia mmoja au nyingine yanarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Nchi hii ni yetu sote na unapoamua kuamasisha maendeleo ya nchi kwa wananchi na ukasikilizwa basi ni vyema pia ukawa tayari kukubali kukosolewa!
Asanteni,
Mwanaharakati wa mageuzi ya maendeleo ya nchi.
Simu
0784844940
RUSHWA ADUI WA HAKI MPAKA LINI?
Submitted by Mwananchi on Thu, 2007-01-25 13:02. RushwaJina
ALEXANDER HAULE
Maoni
RUSHWA:
Maoni yangu jamani tuipinge rushwa kwani ni adui wa haki.Utakuta familia inateseka kufuatilia mirathi mahakamani miaka 2 bila mafanikio,mara watakwambia faili lenu halionekani,mara ooh bado halijafika,yaaani hatuwaelewi hiki chombo kimeweka kwa madhumuni gani ?kutetea wanyonge au kuwakandamiza kabisa?
ALAFU SIONI KABISA KAZI WANAOIFANYA HAWA TAASISI YA KUZUIA RUSHWA(PCB),SIJUI WANAOGOPA AU HAWAWEZI MAJUKUMU YAO?
Simu
0713237512
ubaguzi
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-23 11:09. UbaguziJina
andrew R.Chale
Maoni
NI SWALA LA WADAU WA MASWALA YA UKIMWI KUANDAA MATAMASHA MBALIMBALI YAHUSIYO UKIMWI.Mara nyingi wamekua wakijitokeza wakilatibu kufanikisha matamasha haya NAKUPELEA KUACHA WENGINE hususani watoto yatima wazazi wao walio kufa kwaAJALI,TB,nk bali si kwaukimwi.hapa nimeonelea kutoa maoni yangu kwa uchungu.utakuta wadau wanatangaza matamasha yawatoto yatima wazazi wao walikufa kwa UKIMWI KWAKWELI WENGINE WANAUMIA SANAA.naomba waache
Simu
0717049824
NGO'S
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-16 15:11. HakiJina
CHILLAH.
Maoni
NGO'S kuongozwa na wakuu wa idara mbalimbali serikalini ni kitendo cha kurudisha nyuma maendeleo ya jamii kwani kinazuia haki kwa watu wa tabaka la chini wenye uwezo wa kuendesha miradi.
Simu
0755-162952
USALAMA WA ABIRIA UBUNGO BUS TERMINAL
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-16 11:49. MazingiraJina
Kasele Kwikima
Maoni
Licha ya jiji kutoza sh. 200 Kwa kila abiria na wasindikizaji kwa ajili ya huduma zote ndani ya kituo hicho lakini wameshindwa kuwajali wadau wao hao kwani hakuna mahali salama kwa mvua na jua kwani mara ukatapo tikiti unatembea umbali mrefu juani, katika mvua au tope bila kizuizi chochote. Sehemu pekee yenye paa ni sehemu ya kushushia abiria umbali wa kilomita 0.8 toka magari yaendayo dodoma, morogoro, tanga, iringa, mbeya na sehemu kadhaa. Abiria waendao arusha moshi tu ndio wanaweza kunufaika na eneo hilo. Tatizo lingine ni utozaji ada wakati wa kutoka. Nilimsindikiza mtu kwa kutumia usafiri wa taxi. Kisha taxi ile kuondoka. Nilisubiri kwa muda wa nusu saa basi la iringa liondoke nihakikishe msafiri ameondoka. Mfukoni nilibaki na sh. 400 Tu nauli ya kunirudisha nyumbani mbagala charambe. Nilipofika getini nikadaiwa sh. 200 Ili nitoke. Sikuwa nayo kwani nauli ya mbagala kwa sasa ni sh. 300. Ilibidi mtoza ada anipitishe kwa sh. 100 Bita kunikatia tikiti anisaidie. Ilikuwa ni rushwa na nathubutu kutamka nilitoa rushwa ili nitoke.
Simu
0773 833383
rushwa
Submitted by Mwananchi on Mon, 2007-01-15 10:22. RushwaJina
juma richard okumu
Maoni
kwa kweli suala la rushwa limekuwa ni suala kubwa sana kwa sababu linagusa jamii nzima mfano kwenye vituo vya afya na vituo vya polisi kumekuwepo na vitendo vya rushwa kwa maana hiyo tunaomba serikali ihangalie suala hilo.hasa hapa kwetu musoma na sehemu mbalimbali tanzania.
Simu
Wasomi Wa Tanzania Wanatakiwa!
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-09 10:52.Jina
Michael Paul
Maoni
mimi ninashanga kwa wasomi watanzania kukimbilia nje, Wakati nci yetu ndio imewasomesha, Je serikali haiwatambui au? Kwani ni kupoteza hela za serikali kuwasomesha watu ambao hawaitumikii nchi yao. Ninaiomba serikali iangalie jinsi ya kuwapata wasomi hao ili waitumikie nchi yao.
