waajiri wasiwazuie wafanyakazi wao kujiendeleza kielimu
Submitted by Mwananchi on Sat, 2006-08-26 18:42.
Ajira | Elimu
Jina
Pwani Mwankanda, wa Kiwira, Tukuyu.
Maoni
Tupo kwenye dunia ya utandawazi,sayansi na tekinolojia. Dunia inayo hitaji watu wenye elimu ya kutosha. Lakini, kitu cha kusikitisha ni kwamba, kuna baadhi ya taasisi za serikali na za binafsi hapa tanzania zinawazuia wafanyakazi wake wasijiendeleze kielimu. Viongozi wa taasisi hizi wamekuwa wakiweka vikwazo vingi kwa mtu anaye taka kujiendeleza kielimu. Hii yote inasababishwa na viongozi hawa kuwa na woga wa kupoteza madaraka kwa vijana wenye nia, ari na uwezo wa kujiendeleza kimasomo. Mimi naona serikali itafute maoni toka kwa wafanyakazi,ili kubaini viongozi wenye tabia ya kuzuia wafanyakazi wao wasijiendeleze kielimu. mara watakapo bainika viongozi hawa wafukuzwe kazi, kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu.
Simu
0741663701
