Home Jaqueline Angel Lekei Mama Nancy Ambokile Rose Kevin Thomas Angelina Khamis Anato Emanuel honorath Samahani Ramadhani Lilian Sospeter Happiness Sakina Samuel Nasra Richard Sulemida Juma Hassan Mary Magari Mwaabu Fatuma Abdalla

Mimba kwa wanafunzi.

|

Jina

Soko - Kitangiri

Maoni

Nasikitika sana kwamba mtoto wa kike anaepata ujauzito akiwa shuleni hufukuzwa shule hivyo anakatisha masomo na matarajio yake ya baadae kwake ndio inakua mwisho lakini tukumbuke kua huyu mtoto anaepata ujauzito hawi pekeake kwenye hio starehe wanakua watu wawili yani msichana na mvulana. inakuaje basi afukuzwe msichana pekee nahuyu mvulana aendelee kusoma nafikiri tufungue macho tuone kama watu hawa wameshiriki tendo hilo basi wote wafukuzwe maana bila mvulana msichana huyo asingepata huo ujauzito. Wakati umefika kuwaendeleza hawa wanafunzi kama hio haiwzekani basi wavulana waalimu wafanyakazi hata walinzi nao pia wafukuzwe kazi wanazozifanya kama mtoto huyu wa kike anae achisha masomo yake.Tukumbuke kua kupata ujauzito sio chanzo cha kukosa elimu basi waendelee mara baada ya kujifungua ni vizuri kumpa haki ya msingi ya elimu mtoto huyu wa kike ili wsiwe tegemezi kwa maisha yake hapo baadae. Naomba viongozi wetu tuliangalie suala hili kwa mara nyingine kwani bila kufanya hivyo kutakua hakuna viongozi wakike wa nyadhifa mbalimbali hapo baadae kwani wengi wao watakua hawana elimu ya kutosha. Hvi tunakubali kwamba wanawake waendelee kunyanyasika mpaka lini? Nasema tusikubali kunyanyasika tuna uhuru wa kusema 'NO" pale ambapo hatutaki kudharauliwa kunyanyasika nasi pia tupewe heshima hata sisi ni binadamu kama hao wanaume.

Simu

Barua pepe

Vote Result
----------