Home Jaqueline Angel Lekei Mama Nancy Ambokile Rose Kevin Thomas Angelina Khamis Anato Emanuel honorath Samahani Ramadhani Lilian Sospeter Happiness Sakina Samuel Nasra Richard Sulemida Juma Hassan Mary Magari Mwaabu Fatuma Abdalla

Mikopo kwa Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu

Jina

Respicius Didace

Maoni

Suala la mikopo kwa wanafunzi wa taasisi za Elimu ya Juu sasa hivi ni tatizo ambalo limetawala vyombo vya habari. Ni maoni yangu kuwa kabla ya kusema kuwa wanaofaa kupata mkopo ni wale wanafunzi wenye DIVISION ONE (Wanaume) au DIVISION ONE na DIVISION TWO (Wanawake)ni lazima tufuatilie huko vyuoni kuona kama hayo matokeo ya kidato cha sita yana uhalisia katika matokeo ya vyuoni. Hapa namaanisha kama ni kweli waliopata DIVISION ONE huendelea kuongoza )vyuoni. Mimi naamini kuwa kuna wanafunzi wanapata madaraja ya chini kulingana na aina ya shule wanazosomea au kwa sababu nyingine mbalimbali, hawa wanapokuja vyuoni pengine na DIVISION TWO au THREE zao hufanya vizuri sana hata kuliko wale wa DIVISION ONE. Kutoa mikopo kwa madaraja kutawakosesha watoto wa walalahoi haki yao yamsingi ya elimu. Nadhani pia, ni kuwahukumu bila kuwasikiliza. Naamini siku moja tutakuja kuulizwa tulisema nini kuhusu haya. Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Simu

Barua pepe

Vote Result
----------