Home Jaqueline Angel Lekei Mama Nancy Ambokile Rose Kevin Thomas Angelina Khamis Anato Emanuel honorath Samahani Ramadhani Lilian Sospeter Happiness Sakina Samuel Nasra Richard Sulemida Juma Hassan Mary Magari Mwaabu Fatuma Abdalla

Rushwa CHUO KIKUU

Jina

Eliya Wilbert

Maoni

Ninapenda kutoa maoni/malalamiko yangu kuhusu RUSHWA ya kupata vyumba inayoendelea pale CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM. Kwa kweli ni AIBU kwa wanavyuo KUUZIWA vyumba kwa bei inayoanzia 200,000/ hadi 500,000/ kwa njia isiyo halali. Ninasema hivyo kwa sababu jambo hili limetokea katika semister hii inayoendelea sasa, ma-warden wa mabweni wanadiriki KUWAUZIA wanafunzi vyumba hivyo ambavyo ni HAKI YAO kuvipata kwa taratibu zilizowekwa na utawala wa chuo. Tena kuna kila dalili za UCHAFU huu kuendelea katika semister ijayo. Ninawashauri HAKI ELIMU kufuatilia ninyi wenyewe tena hata kwa kuwahoji baadhi ya wanafunzi hasa wanaoishi HALL VII. Kama wanafunzi hawa watakuwa viongozi hapo baadae, tutegemee RUSHWA kutokuisha Tanzania. Kwani pale walipo wanachukua kozi ya KUTOA NA KUPOKEA rushwa, na hasa ukizingatia kuwa hakuna anayejali wala kufuatilia suala hili. Tunawaomba sana mfuatilie jambo hili na kulifikisha kwenye vyombo vya habari ili kuliokoa taifa letu na mdudu huyu hatari aitwaye RUSHWA.

Simu

Barua pepe

eliyawill@yahoo.com
Vote Result
----------