Mazingira
Submitted by Mwananchi on Fri, 2006-11-03 10:03.
Mazingira
Jina
Godlove Mtengela
Maoni
Maoni yangu ni kuhusu Mazingira, mimi kwa mtazamo wangu suala la mazingira linaniumiza sana, Maana nyumba hizi tunazoishi ni chafu sana ndio maana hata magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu haviwezi kwisha kama suala hili halitatiliwa mkazo maalum. Sioni sababu kwamba kweli Serikali imeshindwa kabisa kudhibiti suala hili la uchafu kila sehemu, kuna haja gani kuwa na Balozi, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa, Diwani, Mbunge nk..., Balozi anashindwa nini kupitia zile nyumba zake kumi na kuhakikisha zinakuwa safi? Inawezekana kabisa kwamba hawezi kufuatilia kwa sababu nyumba zao ndio zinazoongoza kwa uchafu. Huwa napata shida sana kuona uchafu umezagaa kila sehemu, Watanzania tumeshindwa tumeshindwa kweli kudhibiti suala la uchafuzi wa mazingira? utakuta baadhi ya nyumba mitaani maji machafu yanatiririshwa barabarani. Ni kero kweli kwangu binafsi.
