UBAGUZI
Submitted by Mwananchi on Tue, 2006-11-28 08:45.
Ubaguzi
Jina
ELIA MWANGA
Maoni
Mimi nafikiri kwamba bado swala la ubaguzi limekithiri katika nchi yetu ya Tanzania.Ubaguzi unajithihirisha wazi katika ajira, elimu na katika nyanja nyingine za kijamii. Katika swala la ajira bado kigezo kikubwa cha kupata ajira imekuwa ni kujuana na wala si sifa mtu alizonazo.Na haya yamekuwa yanafanywa na viongozi wakubwa tu ambao wako madarakani. Katika swala la elimu bado watoto wa maskini tumekuwa tukibaguliwa hasa katika elimu ya juu.Swala la serikali kutoa mkopo kwa asilimia sitini ni kuwafukuza watoto wa maskini wasio na uwezo wakujilipia.Viongozi ambao wapo serikalini hawana wasiwasi kwani wao kwa kipato chao asiilimia sitini sio tatizo.
