Home Jaqueline Angel Lekei Mama Nancy Ambokile Rose Kevin Thomas Angelina Khamis Anato Emanuel honorath Samahani Ramadhani Lilian Sospeter Happiness Sakina Samuel Nasra Richard Sulemida Juma Hassan Mary Magari Mwaabu Fatuma Abdalla

UCHANGIAJI WA ELIMU YA JUU KWA 40%

Jina

Jonas J.Kimati

Maoni

Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha kilimo Sokoine.Kinachoniuma ni kuona wanafunzi wanateseka kuhusu suala zima la mikopo hasa kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu.Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanalipiwa 60% ya garama zote ikiwa ni ada,malazi,chakula na mengineo.Je,hizo 40% watapata wapi huku angali ni watoto wa wakulima wenye kipato duni?Mfano,ada wanayotakiwa kuongeza ni wastani wa laki tano.Si hayo tu,tumejionea wenyewe ni jinsi gani wanafunzi wa mwaka wa kwanza wananyimwa malazi baada ya kufunguliwa chuo tarehe 08/01/2007 wakitakiwa kukamilisha ada kwanza. Ninachoweza kusema mimi,kulikuwa na utaratibu mbovu wa taarifa kuhusu ushirikishwaji uchangiaji wa gharama za elimu ya juu kwa 40%.Wazazi wengi hawafahamu kuhusu hilo na watakaomia ni wanafunzi.Inabidi bodi isahau kuhusu uchangiaji wa elimu na itoe mkopo kwa 100%,mwaka ujao wa masomo iandae programu nzuri na kila atakayechukua fomu za kujiunga na chuo chochote ajue atachangia kwa asilimia fulani.

Simu

0713803083

Barua pepe

jonskimati@yahoo.co.uk
Vote Result
----------