USALAMA WA ABIRIA UBUNGO BUS TERMINAL
Submitted by Mwananchi on Tue, 2007-01-16 11:49.
Mazingira
Jina
Kasele Kwikima
Maoni
Licha ya jiji kutoza sh. 200 Kwa kila abiria na wasindikizaji kwa ajili ya huduma zote ndani ya kituo hicho lakini wameshindwa kuwajali wadau wao hao kwani hakuna mahali salama kwa mvua na jua kwani mara ukatapo tikiti unatembea umbali mrefu juani, katika mvua au tope bila kizuizi chochote. Sehemu pekee yenye paa ni sehemu ya kushushia abiria umbali wa kilomita 0.8 toka magari yaendayo dodoma, morogoro, tanga, iringa, mbeya na sehemu kadhaa. Abiria waendao arusha moshi tu ndio wanaweza kunufaika na eneo hilo. Tatizo lingine ni utozaji ada wakati wa kutoka. Nilimsindikiza mtu kwa kutumia usafiri wa taxi. Kisha taxi ile kuondoka. Nilisubiri kwa muda wa nusu saa basi la iringa liondoke nihakikishe msafiri ameondoka. Mfukoni nilibaki na sh. 400 Tu nauli ya kunirudisha nyumbani mbagala charambe. Nilipofika getini nikadaiwa sh. 200 Ili nitoke. Sikuwa nayo kwani nauli ya mbagala kwa sasa ni sh. 300. Ilibidi mtoza ada anipitishe kwa sh. 100 Bita kunikatia tikiti anisaidie. Ilikuwa ni rushwa na nathubutu kutamka nilitoa rushwa ili nitoke.
Simu
0773 833383
