Uchumi
Uchumi
 Ni kero ya mafuta, nashangaa! Wakati bandari tunayo Tanzania, na mafuta yanatumia bandari yetu hii ya Tanzania lakini utofauti wa bei ukienda na nchi nyengine kama Zambia na Malawi ni tofauti kabisa, wakati Tanzania bei ni ya ghali Zambia bei nafuu kwahiyo hata mkulima wa chini faida ya kilimo anakuwa hana kisa ni kwaajili ya mafuta.
The issue of the fuel problem surprises me! We have a harbour in Tanzania and the fuel passes through our harbour, but the prices in neighbouring countries like Zambia and Malawi are different. In Tanzania it is so expensive compared to Zambia where it is cheap, which makes it hard for a poor farmer to make any profits, and the reason is fuel.
Uchumi
 Kero yangu hasa ni kama sisi wafanya biashara tukitoa mazao Kijijinj tunadaiwa mara mbili ushuru. Aidha tunatoa ushuru Kijijini alafu tukifika Mjini napo tunatoa ushuru vile vile, wakati Serikali ilishatutangazia kuwa ushuru umefutwa. Sasa huu ushuru unatokana na nini? I am disturbed by the fact that as business people transporting farm produce from the rural areas, we end up paying taxes twice. We pay taxes in the village and then we pay again in town, although the government has announced that these taxes have been dropped, so where does this tax come from?
Uchumi
 Kuhusu sisi wabebaji wa mizigo, tunabeba mizigo watu wanatusumbua kenye malipo, tunafanya kazi nzito pesa inakuwa ndogo. Kwahiyo tunaomba wangetusaidia kwa kuwaelimisha hawa tunaowafanyia kazi watuongeze kiasi kichache kwa kazi tunayofanya.
About us porters: we carry luggage, people harass us when it comes to paying, we work hard for very little pay. So we need your help in sensitising the people we work for, so that they can pay a bit more for the kind of job we do.
Submitted by Mwananchi on Fri, 2006-10-20 22:24.
Maisha | Uchumi
MaoniUchumi wa Tanzania unaporomoka kwa kasi kubwa kutokana na ukosefu wa nguvu ya umeme wa uhakika. Madini ya Uranium yanayotengeneza nishati ya nyuklia yanapatikana Tanzania. Natoa wito kwa Wizara ya Nishati na Madini kuwasiliana na nchi kama Iran na Korea waombe kupewa teknolojia ya uzalishaji nguvu za umeme kwa njia ya nyuklia na tutaondokana kabisa na tatizo sugu la umeme linalokabili nchi yetu.
Submitted by Mwananchi on Thu, 2006-10-12 17:29.
Uchumi
MaoniNia njema ya serikali kuweka na kufuata sheria na taratibu zinazosimamia biashara na masuala mengine ya jamii inaeleweka. Lakini baadhi ya hatua za utekelezaji zinapaswa kutazamwa kwa makini. Kwa mfano, mamlaka husika zinapovunja meza na vibanda vya kuuzia maandazi, chapati, samaki wa mafungu waliokaangwa, vilivyopo katika makazi ya watu wa kipato cha chini. Sidhani kama serikali imeandaa eneo maalumu la kuwakusanya wauza chapati, maandazi na samaki wa mafungu, wa jiji la Dar es Salaam. Wengi wa wauzaji hawa ni akina mama na binti zao. Ni ukweli ulio dhahiri kwamba kwa biashara hizo wanalipa kodi za nyumba, kusomesha watoto na kutunza familia zao. Machinga wametengewa maeneo japo hayatoshi na hayana huduma muhimu. Lakini hawa akina mama wanapovunjiwa soko walilotengewa la chapati, maandazi na samaki wa mafungu liko wapi? Miradi ya TASAF haiwezi kuchukuliwa kuwa tayari imeleta neema kwa watu maskini. Si kweli. Na kama italeta neema, ni baadaye. Neema hiyo haijaonekana bado. Kuwavunjia akina mama hawa ni kuvunja tumaini lao pekee la kipato. Na si kwao tu bali wakazi wengi wa maeneo ya aina hii, mfano Tandika, Mwananyamala, Mbagala, Tabata, Buguruni na mengineyo, hutegemea sana kitoweo cha bei nafuu, wanachoweza kukimudu kutoka kwa wafanyabiashara hawa wadogo. Nia ya serikali ni njema, lakini sidhani kama kero kuu inayowapata Watanzania na kuwakosesha usingizi ni hizi meza na vibanda vya chapati, mchicha, samaki na viazi mbatambata(chips). Wanaumizwa zaidi na uporaji wa mabilioni ya fedha za nchi yao na ufisadi mkubwa uliochangia kuwafikisha baadhi yao katika hali hii ya kutegemea biashara za samaki wa mafungu, mchicha na maandazi. Walikwisha jeruhiwa vya kutosha kwa miaka mingi. Pale sheria zilipokuwa zikimilikiwa na wenye fedha. Na pale polisi na maafisa wa serikali walipogeuka kuwa majambazi au kushirikiana na majambazi. Wanateswa na mgao wa umeme ambao kwa kiasi kikubwa, licha ya tatizo la mvua, umesababishwa na ufisadi wa watawala wao. Watanzania wengi walio maskini walifikia mahali pa kukata tamaa na kupoteza matumaini. Kikwete alichangia kufufua mioyo yao. Sasa ningeiomba serikali isiwazidishie machungu hawa Watanzania walio maskini kwa kuwavunjia hata lile tegemeo lao la kipato, japo ni dogo na lisilo rasmi, lakini linawaokoa wao na watoto wao; hasa kwa yale maeneo ya makazi ya watu wa kipato ca chini.
Submitted by Mwananchi on Tue, 2006-09-26 03:06.
Uchumi
Maoni...mhh kuhusu suala la uchumi kwa ujumla naona raisi wa awamu hii ya tatu kwani watu wanakosa umeme kwa masaa 12 mwezi karibia wa tatu sasa...shilingi yetu inazidi kushuka thamani ikiwa inasabibishwa pia na ukubwa wa serikali iliyoko madarakani na sera mbovu kwa ujumla za raisi aliyeko madarakani...hii yeto mwananchi wa kipato cha chini ndiye anayetwishwa huu mzigo mkubwa kwani hao wakubwa wana majereta wote kwa hiyo hawaoni karaha ya kutokuwepo kwa nishati muhimu kama umeme...
|