Kilimo
Lekei, Same
Ardhi | Elimu | KilimoMimi napenda kwamba wafugaji watengewe maeneo maalum ya kufuga ili waweze kuondokana na hali ya migogoro ya wakulima. Na jamii hiyo hiyo ya wafugaji apewe nafasi ya kielimu.
I would like the pastoralists to be given their own areas dedicated to grazing cattle, so that we can end this state of conflict with farmers. And these pastoralist people should be given opportunities to education.
Ramadhani, Bagamoyo
KilimoSerikali inazungumzia sana kilimo kwenye siasa lakini sio kwenye utekelezaji. Kwa hiyo utakuta wakulima wengi sana wanafanyakazi lakini hawasaidiwi, wengi tunalima lakini kumuona bwana shamba aje shamba kukuuliza au kujua matatizo ya shamba hakuna. Ni mabwana shamba tu wako ofisini kama watu wengine tu wa maofisi.
The government likes to talk about agriculture in politics but not in the implementation. So you find that many farmers are working so hard but they are not getting any assistance, and you will never meet an agricultural officer in the field, so that he could ask you and learn about the problems with farming.
Mary, Dar es Salaam
KilimoMimi ni mkulima wa kilimo hai, napenda sana mazao ya kilimo hai maana yake situmii mbolea na wala situmii madawa ya kiwandani. Ninavyolima kilimo hai nnalinda udongo wangu unakuwa mzuri na pia mazingira siyaharibu kwa kutumia madawa.Mazao haya pia yananipatia kipato nje ya nchi na hapa kwahiyo napata kipato changu na kujiendesha maisha yangu vizuri.
I am an organic farmer, I really like organic produce, I don’t use fertilizers or chemicals from the factory. When I practise organic farming I protect the soil and I don't destroy the environment with chemicals. Farm products are my source of income that enables me to lead a good life.
