Home Jaqueline Angel Lekei Mama Nancy Ambokile Rose Kevin Thomas Angelina Khamis Anato Emanuel honorath Samahani Ramadhani Lilian Sospeter Happiness Sakina Samuel Nasra Richard Sulemida Juma Hassan Mary Magari Mwaabu Fatuma Abdalla

videos

Jonas, Mbeya

Ni kero ya mafuta, nashangaa! Wakati bandari tunayo Tanzania, na mafuta yanatumia bandari yetu hii ya Tanzania lakini utofauti wa bei ukienda na nchi nyengine kama Zambia na Malawi ni tofauti kabisa, wakati Tanzania bei ni ya ghali Zambia bei nafuu kwahiyo hata mkulima wa chini faida ya kilimo anakuwa hana kisa ni kwaajili ya mafuta.


The issue of the fuel problem surprises me! We have a harbour in Tanzania and the fuel passes through our harbour, but the prices in neighbouring countries like Zambia and Malawi are different. In Tanzania it is so expensive compared to Zambia where it is cheap, which makes it hard for a poor farmer to make any profits, and the reason is fuel.

Vote Result
----------

Subi, Lushoto

Swali, kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi. Ni kwanini Tanzania virusi vya ukimwi vinazidi, nchi za wenzetu zinapunguwa? Ningeona serikali ya Tanzania ichunguze nchi za wenzetu wanavyofanya, wafuate mfumo huo na Tanzania.


A question regarding the spreading of HIV/AIDS: why is the infection rate still going up in our country while it is decreasing in the neighbouring countries? Our government should investigate what others are doing and replicate it here.

Vote Result
----------

Josephat, Mtwara

Miundo mbinu ya watanzania inasikitisha kweli, kwasababu miundo mbinu iliopo kwa sasa haikidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu, iwe ya binafsi, iwe ya Serikali. Hivyo tunawaomba wale wanao husika na masuala ya miundo mbinu kukumbuka kwamba na watu wenye ulemavu wapo.

 


The infrastructure for Tanzanians makes me really sad, because it does not consider the needs of the physically challenged people, be it the private or government. We therefore call to all those involved in infrastructure development to remember the disabled amongst us. 

 

 

Vote Result
----------

Donatus, Tabora

Elimu inayotolewa kwa watoto wa kitanzania na hasa katika mpango wa MMEM na MEMCO, uhakikishe kwamba unawahusisha na watoto wote wenye ulemavu hasa wasio ona maana katika mpango huo wanaonekana kusahaulika kabisa.


It should be ensured that the education given to Tanzania children, in particular through MMEM and MEMKWA programmes, includes all the physically challenged children especially the blind ones because in this programme they seem to have been left out.

Vote Result
----------

Janet, Tabora

Eeh kero kubwa ni upande wa sisi wajane unapoachwa na mume wako, unakuta familia ya mume wako ndio inakuja kukunyang'anya mali na kila kitu halafu inakuwacha na watoto yatima utunze mwenyewe. Wakati hao ndugu hawakuchangia chochote katika maendeleo yetu ya mimi na mume wangu.


My biggest concern is about us widows, when you loose your husband you find that the family of your husband comes and takes away the possessions and every thing else, leaving you to take care of the orphans by yourself. Even though they did not contribute in any way to the development of me and my husb

Vote Result
----------

Aisha, Dar es Salaam

Nachangia kuhusu suala la michezo limerudishwa  mashuleni lakini zana za michezo hakuna. Hivyo tulikuwa tunaomba ziletwe zana za michezo mashuleni ili kuboresha michezo.


I would like to talk about the reintroduction of school games yet the sports gears are unavailable. We would like to request that these gears be provided to improve the sports in schools.

Vote Result
----------

Salome, Iringa

Shule za msingi ada zimefutwa, lakini michango imezidi kupita kiasi. Inapofungwa shule kila kichwa cha mwanafunzi ni shilingi elfu sita, michango kila mwezi ni shilingi mia mbili, ambapo yaani hiyo ni kero kwetu sisi wazazi ambapo yaani ni bora ingerudi ada kuliko ile michango ya siku zote.


Primary school fees have been abolished, but the contributions we are supposed to pay are just too much! When the school closes we pay Tsh.6000 per pupil, we pay a monthly contribution of Tsh.200 and this really annoys us as parents. We would actually prefer to pay fees rather than contributions every day.

Vote Result
----------

Mama Hassan, Iringa

Kero yangu hasa ni kama sisi wafanya biashara tukitoa mazao Kijijinj tunadaiwa mara mbili ushuru. Aidha tunatoa ushuru Kijijini alafu tukifika Mjini napo tunatoa ushuru vile vile, wakati Serikali ilishatutangazia kuwa ushuru umefutwa. Sasa huu ushuru unatokana na nini?


I am disturbed by the fact that as business people transporting farm produce from the rural areas, we end up paying taxes twice. We pay taxes in the village and then we pay again in town, although the government has announced that these taxes have been dropped, so where does this tax come from?

Vote Result
----------

Abdalla, Mbeya

Kwa sababu ni mfanyakazi eneo la Stend, kero langu lipo kwa gari zinatoka Tunduma, zinatoka Kiera, zinatoka Chunya zinaishia Mwanjila wakati kuna Stend kuu hapa yakufika watu kuja kupokea ndugu zao, hasa hapa watu wanapata tabu kuja kuwatafuta ndugu zao. Ndugu yako ametoka wapi, ametoka Kiela inabidi apate tabu tena kutoka hapa aende tena Mwanjila kwenda kumtafuta ndugu yake wakati hapa kuna Stend kuu ipo hapa Mbeya.


As I work at the bus stop, I am irritated about the public transport vehicles from Tunduma, Kiero and Chunya that terminates the journey at Mwanjila, whereas there is a main bus terminal here in Mbeya where relatives and friends wait to receive the passengers.

Vote Result
----------

Noel, Iringa

Kuhusu sisi wabebaji wa mizigo, tunabeba mizigo watu wanatusumbua kenye malipo, tunafanya kazi nzito pesa inakuwa ndogo. Kwahiyo tunaomba wangetusaidia kwa kuwaelimisha hawa tunaowafanyia kazi watuongeze kiasi kichache kwa kazi tunayofanya.


About us porters: we carry luggage, people harass us when it comes to paying, we work hard for very little pay. So we need your help in sensitising the people we work for, so that they can pay a bit more for the kind of job we do.

Vote Result
----------


Syndicate content